Rais wa Marekani, Donald Trump amewasiliana kwa njia ya simu na Rais wa Urusi Vladimir Putin kujadili namna ya kutatua migogoro mbalimbali inayoikabili dunia kwa sasa.
Putin na Trump wameongea kwa mara ya kwanza baada ya majeshi ya Marekani kuipiga Syria ambayo Putin anayaunga mkono majeshi ya Syria.
Idara ya mawasiliano ya White House imeeleza kuwa Donald Trump na Vladimir Putin kwenye maongezi yao, wamekubaliana kuingilia kati vita vinavyoendelea nchini Syria kwa usuluhishi.
Viongozi hao wawili pia wamejadili namna ya kufanya kazi kwa pamoja ili kuliangamiza kundi la IS pamoja na suala la nyuklia la Korea ya Kaskazini.
Haya ni maongezi ya kwanza kwa viongozi hao wawili wenye nguvu zaidi duniani, tokea Trump alipoishambulia Syria inayoungwa mkono na Urusi.