Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesamehewa na Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge la Tanzania baada ya kukiri makosa yake.

Kamati hiyo leo imewasilisha bungeni taarifa za matukio mbalimbali ambazo imezifanyika kazi ikiwa ni pamoja na kuwaita na kuwahoji wahusika kwa kukiuka kanuni za bunge nje na ndani ya bunge hilo.

Miongoni mwa taarifa hizo ni pamoja na ile ya kuingilia uhuru wa bunge kosa lililofanywa na Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka bungeni, viongozi hao wate wawili wamesamehewa kutokana na kukiri makosa yao na kuliomba radhi bunge la Tanzania.

Kamati hiyo ya Maadili ya Bunge imemsamehe Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe baada ya kukiri kutoa lugha ya kudharau mamlaka ya bunge.

Kwa upande mwingine Kamati ya Maadili ya Bunge imemuadhibu Mbunge Halima Mdee  kutohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyosalia kwa kudharau mamlaka ya bunge.

Pia Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya amepewa karipio kali na Kamati ya Maadili ya Bunge kwa kosa la kudharau Mamlaka ya Spika wa Bunge.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *