Muigizaji nyota wa Bongo Movie, Wema Sepetu leo amepandishwa tena kizimbani katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kesi ya matumizi ya dawa kulevya.
Wema alifika mahakama hapo akiwa na mama yake mzazi pamoja na baadhi ya waigizaji wenzake waliomsindikiza kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo ya tuhuma za kutumia na kukutwa na madawa ya kulevya.
Katika kesi hiyo upande wa Jamhuri umekamilisha upelelezi wa kesi hiyo inayomkabili muigizaji huyo.
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ameahirisha kesi hiyo mpaka Juni 1, mwaka huu ambapo mahakama itasikiliza maelezo ya awali ya upelelezi huo.
Katika kesi hiyo Wema na mwenzake wanakabiliwa na makosa matatu yanayohusiana na matumizi ya madawa ya kulevya aiana ya bangi.
Wema Sepetu ni miongoni mwa wasanii wa Bongo waliotajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wanaotumia dawa za kulevya.