Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli leo anatarajia kuwaongoza wakazi wa Moshi katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambazo kitaifa zinafanyika leo mjini Moshi.

Rais Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo zinazofanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU), ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani hapa iliyoanza juzi.

Kwa mujibu wa Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, Rais Magufuli atazungumza na wafanyakazi wote nchini kupitia sherehe hizo kwenye uwanja huo.

Pia Rais Magufuli atatoa maelekezo kuhusu kilio cha vyama vya wafanyakazi ambacho ni pamoja na kukosekana kwa mikataba ya hali bora kazini.

Mkuu wa mkoa huyo amewataka wafanyabiashara watumie fursa hii kufanya biashara zako kwa ukarimu na uaminifu mkubwa ili kuwavutia wageni wanaoingia Moshi na watakaoendelea kuja.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *