Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako amesema suala la uhakiki wa vyeti feki nchini tangu Tanzania ipate uhuru ni mara ya kwanza zoezi la uhakiki kufanyika huku akisema suala hilo bado linaendelea.

Profesa Ndalichako, ameyasema hayo mjini Dodoma wakati wa kumkabidhi Rais Magufuli taarifa ya majina ya watumishi wa umma wenye vyeti feki.

“Mheshimiwa Rais, suala la uhakiki wa vyeti umefanyika kwa mara ya kwanza, tangu nchi yetu ilipopata uhuru, tunakupongeza sana kwa kuonyesha uongozi thabiti kwa vitendo. Kwakweli huna kigugumizi katika kufanya maamuzi, na tunakupongeza sana.

Mheshimiwa Rais, wizara yangu imetekeleza maelekezo ya serikali kwa kuhakiki vyeti vya kidato cha nne, cha sita na vyeti vya ualimu katika ngazi ya cheti na stashahada kwa watumishi wa umma nchini,”.

 “Kwa hiyo naomba mnisikilize vizuri, tumehakiki vyeti vya kidato cha nne na cha sita kwahiyo kwa maneno haya, ngoma bado mbichi maana yake vyeti vya taaluma bado hatuja hakiki.

Aidha Ndalichako aliwaasa wanafunzi wote nchini kusoma kwa bidii, na kuongeza njia zote zimefungwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *