Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki amesema kuwa Uhakiki wa vyeti feki haujahusisha viongozi wa Kisiasa ambao wako serikalini kama vile Mawaziri, Wakuu wa Mikoa na Wilaya.
Waziri huyo amesema hayo leo wakati akikabidhi ripoti ya vyeti feki kwa watumishi wa umma kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli mjini Dodoma.
Pia amesema kuwa viongozi wa kisiasa wao maamuzi yao yataamuliwa na mamlaka ya uteuzi ndiyo watajua ufanisi wa kazi zao na pia katika siasa ni kujua kusoma na kuandika.
Kairuki amesema uhakiki huo ulihusisha kwa wafanyakazi wa sekta za Serikali ambao si wanasiasa ndiyo walihakikiwa kwenye ripoti hiyo.
Kwa upande wake Rais Magufuli amesema kuwa watumishi hao walioghushi vyeti watakatwa mshahara wa mwezi huu, wafukuzwe kazi na wafungwe jela miaka saba.