Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumshambulia mwanamke mmoja na kumsababishia maumivu makali.

Msambatavangu, ambaye alikuwa miongoni mwa wanaCCM waliofukuzwa uanachama katika Mkutano Mkuu Maalum wa chama hicho uliofanyika mwezi Machi, alikamatwa  jana mchana

Kamanda wa Polisi mkoani Iringa, Julius Mjengi, alisema kuwa kiongozi mstaafu anatuhumiwa kutenda kosa hilo wiki iliyopita.

Kamanda Mjengi alibainisha kuwa kiongozi huyo alitenda kosa hilo akiwa na wenzake ambao asingeweza kuweka majina yao hadharani kwani wanaendelea kuwatafuta.

Mjengi alikataa kuweka wazi jina la mwanamke na idadi ya watuhumiwa wengine kwa maelezo kuwa kufanya hivyo kunaweza kuharibu upelelezi unaoendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *