Muigizaji wa Bongo Movie, Yusuph Mlela amemtaka Nay wa Mitego kuheshimu kazi za watu wengine na siyo kuongea yasiyomuhusu.

Mlela amesema kwamba Nay anapaswa kuacha kufuatilia mambo  yasiyo muhusu na aendelee na shughuli zake za uimbaji au akae pembeni na masuala ya movie kwani siyo upande wake.

‘Mimi namuomba sana Nay ajiheshimu sana, asiingilie kazi za watu ambazo hazimuhusu. kama yeye ameshajiweza kwenye suala la kipato basi akae pembeni atuache wengine tutafute riziki”.

“Sawa mimi na yeye tunaweza tukawa  hatulingani labda kiuwezo na kimaisha kwa sababu yeye anaona tayari amekwisha rizika, ndio maana namuomba tupande ulingoni ili tuheshimiane. Mimi kama ningekuwa naimba ningeingia studio nikatengeneza wimbo wa kumchana lakini kwa vile kazi zetu haziingiliani ndiyo maana nasisitiza ki Hip hop tuu tuingie ulingoni ili heshima iwepo tuache maneno maneno”.

Pia Mlela amekanusha kauli ya kuitwa mtoto wa kike na Nay na kumgeuzia kibao kwa kudai mtu anayeisifu mvua sana huenda ikawa imemnyea ndio maana kutwa anaizungumza kauli ya kumfananisha na mwanamke.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *