Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Pomnbe Magufuli leo atapokea taarifa ya kazi ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma katika ukumbi wa Chimwaga mkoani Dodoma.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu imesema Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki ndiye atawasilisha taarifa hiyo kwa Rais.

Kazi ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma iliendeshwa na Serikali kuanzia Oktoba mwaka jana.

Rais Magufuli wakati akizindua majengo ya hostel za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alisema anasubiri ripoti ya Watumishi wa serikali ambao wanavyeti feki ili awashughulikie huku akidai kuna watu zaidi wa elfu tisa wana vyeti feki.

barua

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *