Marekani imeahidi kuongeza nguvu dhidi ya Korea Kaskazini, kuilaazmisha kurejea kwenye meza ya mazunguzo kuhusiana na programu yake ya nyuklia.

Msimamo huo wa Marekani, ambao ulionekana kuashiria utayarifu wa kumaliza njia zote zisizo za kijeshi licha ya onyo za mara kwa mara kwamba njia zote zinazingatiwa.

Taarifa iliotolewa na waziri wa mambo ya nje Rex Tillerson, waziri wa ulinzi Jim Mattis na Mkurugenzi wa idara ya Intelijensia Dan Coats, iliielezea Korea Kaskazini kama kitisho kikubwa cha usalama wa taifa na kipaumbele cha sera ya kigeni.

Mmoja wa maseneta waliohudhuria mkutano wa ikulu Chris Coons kutoka chamacha Democrat, alisema wabunge hawakupatiwa maelezo kuhusu njia makhsusi za kijeshi au kuombwa kuidhinisha shambulili, lakini aliwaambia waandishi habari kuwa malezo waliopewa yalikuwa ya busara.

Kitisho cha nyuklia na makombora kutoka Korea Kaskazini, kinaelezwa kuwa changamoto nzito zaidi ya kiusalama inayoukabili utawala wa rais Donald Trump kwa wakati huu. Trump ameahidi kuizuwia Korea Kaskazini kuwa na uwezo wa kuishambulia Marekani kwa kutumia kombora na nyuklia, uwezo ambao watalaamu wanasema inaweza kuupata baada ya mwaka 2020.

Tarifa ya maafisa hao wa juu wa serikali ilisema mkakati wa rais unalenga kuishinikiza Korea Kaskazini kuvunja programu zake za utengenezaji na uenezaji wa nyuklia na makombora ya masafa marefu na ya kati, kwa kuimarisha vikwazo vya kiuchumi na kuchukuwa hatua za kidiplomasia pamja na washirika wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *