Naibu Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla amempongeza mwanamuziki Ray C kwa wimbo wake ‘Unanimaliza’ aliouachia hivi karibuni.
Dk. Kigwangalla ametoa pongezi hizo kupitia akaunti yake ya Instagram mapema leo baada ya kuguswa na wimbo huo mpya.
Dk. Kigwangalla ameandika “Mimi kama Naibu Waziri wa Mambo ya Wanawake, kama balozi wa wanawake na kama Daktari niseme nimefurahishwa na kuvutiwa sana na jitihada anazofanya huyu dada Ray C nimeguswa na wimbo wake wa unanimaliza.
Pia ameongeza kwa kuandika “Nimeona nimuunge mkono kwa kuwaomba wadau wote ambao mmekuwa naye siku zote mfahamu kuwa sasa anahitaji support yetu zaidi kuliko wakati wowote ule. Tumuunge mkono kwa dhati. Mungu atatujaalia kheir kwenye maisha yetu pia.
Ameendelea kusema “Hakuna aliyekamilika sote tuna vipindi vyetu vya kuanguka Na kwa hakika tunahitaji ‘a second chance’ kila siku za maisha yetu! Hakuna anayeweza kujisimamia mwenyewe, sote tunahitaji mtu mmoja wa kutushika mkono na kutunyanyua pindi tunapoanguka.
Mwisho amemaliza kwa kusema “Kila la kheir Ndg. Rehema Chalamila. With our support, even the sky is not the limit! Keep on moving, keep on believing.
Dkt. Kigwangalla ni miongoni mwa wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva kutokana na posti zake za kusifia baadhi ya wasanii ambapo wiki chache zilizopita alimwagia sifa mkali wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz baada ya kuzindua Perfume yake ‘Chibu Perfume’.