Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema ameagiza nyumba zaidi ya 200 zilizopo kwenye bonde eneo la Majohe zibomolewe bila fidia.
Bi. Sophia amesema, ujenzi wa nyumba hizo unaathiri mtiririko wa maji kwani ziko kwenye mkondo maji na husababisha maji kufurika na kuharibu miundombinu hasa barabara ya Pugu-Majohe.
Mkuu wa Wilaya huyo amewashangaa wananchi walionunua viwanja kwenye eneo hilo na kujenga huku wakiona ni eneo la bondeni na kuamuru ujenzi usitishwe mara moja.
Bi. Sophia Mjema amesema kutoka kwenye bonde hadi mita 60 pande zote haitakiwi mtu kujenga na watakaojikuta wapo ndani ya umbali huo waanze kubomoa wenyewe.
Pia Mkuu wa wilaya huyo ametoa rai kwa wananchi kuacha kununua na kujenga maeneo hatarishi ya mabondeni kwani uhathiriwa na mafuriko.