Muigizaji na mchekeshaji nchini, Steven Mangere ‘Steve Nyerere’ amesema kuwa kitendo cha waigizaji kujiingiza kwenye siasa ni chanzo cha tasnia ya filamu nchini kupoteza dira nchini.
Amesema hayo ikiwa ni siku chache tangu kufanyika maandamano ya baadhi ya wasanii wa filamu kuishinikiza serikali kuwaondolea kodi katika filamu zao.
Pamoja na kuhakikisha inakusanya pia kodi za filamu za nje ambazo zinakuwa zinapakuliwa katika mitandao kitu kinachopelekea kuua soko la ndani la filamu za Bongo.
Pamoja na hayo Steve Nyerere ameongeza wapo wasanii wa filamu ambao wameweza kutenganisha siasa na filamu na kwamba hao ni wale ambao wamebahatika kuvaa kofia hizo mbili ndio maana wametumia busara zao kutotumika kwenye maandano ya watu wachache.
“Unajua pamoja na siasa kuna watu pale Bongo Movie wana kofia mbili mbili mfano mimi niliwahi kugombea Ubunge wa Kinondoni kwa hiyo lazima najua nini nafanya.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa Irene Uwoya ni Mbunge pale na anayo nafasi yake ndani ya chama ikitokea bahati mbaya mbunge wa viti maalumu akaanguka yeye ndiye atakayeziba pengo.
Alimalizia kwa kusema kuwa Wema Sepetu na harakati aliozonazo sasa hivi na ndio maana hata ukiangalia kwenye maandamano watu waliyoyafanya wao walikaa pembeni siyo kwamba siyo wasanii , hapana ni wasanii ambao wamejitambua na hawataki kutumika kwa maslahi ya watu.