Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amepiga marufuku hospitali za umma nchini kulipisha wagonjwa wanaopima maralia.

 Amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya Malaria duniani mjini Dodoma leo.

Waziri Ummy amesema kuwa vipimo vya maralia ni bure na pia mgonjwa asilipishwe fedha kwa dawa za mseto.

Ummy amewataka wananchi kushirikiana na serikali kuwafichua wahudumu wa Afya ambao watawalipisha fedha pindi watakapo kuwa wanapima huduma ya Malaria kupitia kipimo cha MRDT ama watakapohitajika kupewa dawa ya mseto (ALUU),.

Pia amezionya maabara binafsi ambazo  zimekuwa zikifanya kazi zake kwa kuangalia zaidi fedha badala ya maisha ya mtu kama kuwaambia wana maambukizi ya malaria wakati hawana.

Kwa upande mwingine waziri Ummy amesema takwimu kutoka katika vituo vinavyotolea huduma za afya zinaonyesha takribani watu milioni 12 wanaugua ugonjwa huo kwa mwaka ambapo katika tafiti hizo mkoa wa Kagera, Geita na Kigoma ziliweza kuonekana na viwango vikubwa vya maambukizo kwa mwaka 2015 na 2016.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *