Rais mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kiwete amesema kuwa Suala la elimu kwa wote bado ni changamoto kubwa hususani kwa nchi masikini na za kipato cha wastani.

Kikwete ambaye alikuwepo Washington D.C kwenye mkutano wa ufadhili wa elimu wa mkakati mpya uliozinduliwa mwaka jana kwa nchi za Afrika “The Pioneer country Initiative” baada ya kuzuru nchi 14 zilizo katika mradi huo wa awali.

Dkt. Kikwete amesema alichobaini kuna matatizo makubwa matatu kwenye nchi masikini na nchi za uchumi wa kati ambapo vijana wengi wanaostahili kuwepo mashuleni hawapo mashuleni.

Pia amesema kuwa wanafunzi waliopo mashuleni wengi wao hawamalizi masomo yao na jambo la tatu watu wanaomaliza masomo yao hawapati elimu wanayostahili kuipata.

Kikwete ameongeza kuwa tume imependekeza nchi husika zinapaswa kufanya mageuzi katika mifumo yao ya elimu ili kuweza kupata matokeo chanya katika sekta hiyo ya Elimu katika nchini zinazoendelea.

Nchi hizo ni pamoja na Botswana, Chad, Congo Brazzaville, Cote d’voire, Ethiopia, Gabon, Ghana, Malawi, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Tanzania, Tunisia na Uganda.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *