Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekanusha kuwepo kwa taarifa zinazotoa tahadhari dhidi ya matumizi ya mafuta ya alizeti kutokana na mbegu za alizeti kuchafuliwa na sumukuvu.

Akizungumza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Mkurugenzi wa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo amesema kuwa kutokana na utafiti uliofanyika na wataalam kwa kutumia mashudu na mbegu za alizeti utafiti huo hautoshelezi kuthibitisha kuwepo kwa sumu hiyo ambayo ni hatari kwa walaji.

Sillo amesema kuwa wananchi waendelee kuyatumia mafuta hayo hasa yaliyothibitishwa na mamlaka hiyo bila wasiwasi na kuwa bado wanaendelea kufanya uchunguzi kuhusiana na taarifa ya utafiti huo.

alizethi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *