Mkuu wa  Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa yupo tayari kwa mapambano baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kumfungia mwaka mmoja asijihusishe na soka.

Haji Manara amesema hayo baada ya kutolewa  hukumu na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu, Jerome Msemwa ya kumfungia kujihusisha na masuala ya soka.

Manara amefungiwa kutokana na makosa matatu ambayo ni kuituhumu na kuidhalilisha TFF, kueneza chuki za ukabila kwa kudai Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu wake Selestine Mwesigwa kuwa ni Wahaya na viongozi wa zamani wa Yanga na la mwisho kuingilia utendaji wa shirikisho hilo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Manara amefunguka mazito kutokana na hukumu hiyo aliyopewa jana.

“Unazuia na kutonipa nafasi ya kusikilizwa, unanipa hukumu kwa makosa nisiondikiwa katika mashtaka yao..Nipo tayari kwa ajili ya mapambano, tukutane juu”.

Haji Manara amesimamishwa kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja na pia kutakiwa kulipa faini ya Shilingi Milioni tisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *