Mwanamuziki wa hip hop Bongo, Nay wa Mitego amejibu muigizaji Yusuf Mlela baada ya muigizaji huyo kutaka pambano na Nay wa Mitego.
Hayo yameibuka baada ya Nay wa Mitego kuwaita wasanii wa filamu ‘matahira’ kisa kuandamana kupinga biashara ya filamu ‘feki’ za nje ambazo hazilipi kodi.
Rapa huyo amedai hawezi kupigana muigizaji huyo huku akimkejeli kwa kumuita ni mwanamke.
“Nasikia kuna mwanaume/mwanamke yupo Bongo Movie anataka kupigana na mimi, bahati mbaya mimi sipigani na mwanamke hata baba yangu aliniambia mwanamke hapigwi,” alisema Nay kupitia video iliyosambaa mtandaoni.
Pia ameongeza kwa kuandika ,”Naona kuna watu wanashadadia hili suala kwamba tupigane, mimi siwezi kupigana naye labda nitafutiwe mwanaume mwenzangu ili tutengeneze hela lakini kunipiganisha na mwanamke ambaye wamepoteza marinda hapana.
Baada ya kutangaza anataka kupigana na mimi Bongo Movie wenzake walinipigia simu wakaniambia achana na huyo mtu ni mwanamke mwenzao alishapoteza marinda,”.