Waziri Mkuu wa Jamuri ya Muugano wa Tanzania, Kassim Majliwa amewataka watanzania kuwa watulivu na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili waweze kubaini wahusika wa matukio ya uhalifu yanayotokea nchini ikiwemo utekaji na kutoweka kwa baadhi ya watu akiwemo Ben Sanane.

Amesema hayo wakati wa akijibu swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe katika kipindi cha Maswali kwa Waziri Mkuu bungeni Mjini Dodoma.

Amesema watanzania wanapaswa kuwa watulivu na kuviamini vyombo vya uchunguzi ambavyo vitakuja na majibu yatakayoonesha nini kinachoendelea nyuma ya matukio hayo.

Mbowe alitaka kauli ya serikali kuhusu matukio hayo, ikiwemo kutoweka kwa msaidizi wake Ben Sanane ambaye hadi sasa ni takriban miezi mitano imepita tangu kijana huyo atoweke, lakini akihoji sababu za serikali kutohusisha mataifa mengine yaliyoendelea katika masuala ya kiuchunguzi hususani Uingereza katika kufanya uchunguzi wa masuala ya aina hiyo.

Kwa upande mwingine, Majaliwa amemjibu Kiongozi wa Upinzani kuwa suala la kurusha matangazo ya shughuli za Bunge yalishafikiwa katika Bunge lililopita na serikali itaendelea kuboresha kila wakati namna ya urushwaji wa matangazo hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *