Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kufungua kongamano la maadili  lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata).

Akizungumza kwa niaba ya Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Aboubakar Zuberi Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Bakwata, Sheikh Khamis Mataka, alisema kongamano hilo litafanyika Aprili 24.

Amesema lengo la kongamano hilo ni kujadili mmomonyoko wa maadili uliopo ndani ya jamii hivi sasa.

Pia amesema kongamano hilo la siku moja litafungwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein.

Amesema wengine watakaohudhuria kongamano hilo ni wajumbe wa Ulamaa Taifa, masheikh kutoka taasisi mbalimbali, viongozi wa kidini kanda, mabalozi, wakuu wa vyombo vya usalama na wananchi walioalikwa.

 

Sheikh Mataka alisisitiza kuwa maadili ni muhimu ndani ya jamii na kwamba kwa sasa nchi inakabiliwa na mmomonyoko wa maadili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *