Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May ameitisha uchaguzi mkuu nchini humo ambao utafanyika tarehe 8 Juni mwaka huu.
Bi. May ameliomba Bunge la Commons kuunga mkono pendekezo lake hilo hapo kesho, ambapo ndipo liidhinishwe, litahitaji kuungwa mkono na theluthi mbili ya wabunge.
Amesema Uingereza inahitaji mazingira ya uhakika na uthabiti kufuatia hatua ya taifa hilo kupiga kura kujiondoa kutoka kwa Umoja wa Ulaya mwaka jana.
Bi May amesema kuwa nchi inaungana pamoja, lakini Westminster (Wabunge) hawaungani pamoja.
Uchaguzi mkuu ulikuwa umepangwa kufanyika 2020 lakini waziri mkuu huyo ameamua kuitisha uchaguzi huo mapema mwaka huu.
Lakini akitetea msimamo wake huo mpya, amesema: “Nimeamua kwamba njia pekee ya kuhakikisha uthabiti na usalama miaka ijayo ni kuandaa uchaguzi huu.