Mkazi wa Mbande jijini Dar es Salaam, Asma Juma kuishutumu Hospitali ya Wilaya ya Temeke kumuimbia mtoto mmoja, baada ya kujifungua pacha.

Mwanamke huyo amesema kabla ya kwenda kupewa rufaa ya kujifungua katika hospitali hiyo, alipima kipimo cha ‘ultrasound’ na kuthibitishiwa kuwa ana mapacha.

Asma alisema awali alikuwa akipata huduma za kliniki katika Zahanati ya Serikali ya Mbande, lakini alikuwa amefanya vipimo vya ‘Ultrasound’ katika Zahanati ya binafsi ya Huruma iliyopo Mbande mara mbili na kuthibitishiwa kuwa ana pacha.

“Wakati napelekwa chumba cha upasuaji nilikuwa sina kichaa cha uzazi, siumwi uchungu, siumwi kichwa, siyo kipofu, siyo kiziwi, nasikia kwa masikio yangu na kumbukumbu zote nimezihifadhi kwenye kichwa changu. Ninachotaka ni mtoto wangu,”.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dk Gwamaka Mwabulambo alikiri kuwapo kwa tuhuma hizo na kusema tayari zinafanyiwa kazi na uongozi.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *