Kagera Sugar imeaiandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kulalamikia maamuzi yaliyotolewa na kamati ya saa 72 kwa kuipatia pointi tatu timu ya Simba ikidaiwa wamemchezesha mchezaji mwenye kadi tatu za njano.

Braua hiyo iliyopelekwa moja kwa moja kwa Mtendaji Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa imeandikwa na Mwenyekiti wa klabu hiyo  Hamis Mdaki na kuelekeza malalamiko yao ya kutokubaliana na maamuzi ya kamati ya saa 72.

Hukumu ya kuipatia Simba alama hizo ilitoka juzi usiku baada ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Mohamed Yahya  kutoa maamuzii hayo mbele ya waandishi wa habari na kusema kuwa kamati imethibitisha kuwa Mchezaji Mohamed Fakhi alikuwa na kadi tatu za njano alizozipata katika michezo dhidi ya Prisons, Majimaji na African Lyon.

Hukumu hiyo imeonekana kutokukubalika kwani kamati ilishindwa kupitia ripoti za waamuzi baada ya kuonekana kutofautiana baina ya mwamuzi na kamisaa wa mchezo na kuamua kuwaita waamuzi waje kuthibitisha kama ni kweli Fakhi alipewa kadi ya njano.

Kagera wamemtaka katibu mkuu kuiangalia upya hukumu hiyo kwani wana uhakika kuwa Fakhi alikuwa na kadi mbili za njano na sio tatu kama wanazodai Simba.

Katika mchezo huo wa Kagera walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-1 dhid ya Simba uliochezwa kwenye dimba la Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *