Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo amewataka watumishi wa umma kuzifanyia kazi tafiti zinazofanywa mashirika yasikuwa ya kiserikali.

Jafo amesema kuwa tafiti ambazo zimekuwa zikifanywa na Mashirika mbalimbali ni muhimu sana katika utatuzi wa kero mbalimbali zinazo ikumba jamii.

Ameyasema hayo Mjini Dodoma wakati wa uzinduzi wa ripoti ya sita ya mwaka ya upimaji kujifunza iliyotolewa na Shirika la Twaweza.

Pia Jafo ameongeza kuwa kuanzia sasa mtaalamu yeyote atakaebainika kutofanyia kazi tafiti hizo kwa kuzifungia kabatini atachukuliwa hatua kali kwani Mashirika mengi yamekuwa yakitumia muda mwingi kwa ajili ya kazi hiyo.

Naibu Waziri huyo amesema watayafanyia kazi mapungufu yote yaliyojitokeza katika ripoti hiyo ili yaweze kuwafikia walengwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Twaweza, Aidan Eyakuze amesema kuwa tafiti hizo zinzofanywa na Shirika hilo zinajumuisha nchi mbalimbali barani Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *