Mbunge wa Sumbawanga Mjini (CCM), Aeshi Hillaly amesema kuwa yeye ni miongoni mwa wabunge waliotishiwa maisha na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Ameyasema hayo leo Bungeni mjini Dodoma alipopata nafasi ya kuzungumza na kuchangia bajeti ya waziri mkuu.
Mbunge huyo amesema kuwa mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Dar es Salaam alimtishia masiha mbele ya mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ali Hapi.
‘Mimi Leo nilikuwa sitaki kusema, lakini ngoja tu niseme, nimetishwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, aliniambia nyie wabunge ni wanafiki na nitawashughulikia na nitaanza na wewe, mimi leo Dar naiogopa’.
‘Niko tayari kuhojiwa hapa nimelisema hapa kwa usalama wangu. Alinitisha mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni pale Colosseum Hotel’.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa yupo tayari kuhojiwa juu ya suala hilo kutokana kwasasa anashindwa kusafiri Dar es Salaam kwa kuhofia usalama wake.