Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amesema kuwa watu wanaofanya maandamano dhidi yake ni wabaguzi wa rangi kwasababu walibeba mabango yalioonyesha kuwadharau watu weusi.
Maelfu ya waandamanaji walifanya maandamano baada ya kumfuta kazi waziri wake wa fedha Pravin Gordan.
Maandamano hayo yalipangwa na vyama kadhaa vya upinzani na makundi kadhaa ya wanaharakati.
Wakati huohuo wafuasi wa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma walivuruga hafla ya makumbusho ya aliyekuwa mwanaharakati wa kupambana na ubaguzi wa rangi, Ahmed Kathrada.
Watu hao walianza kuleta uzushi wakati aliyekuwa waziri wa fedha Pravin Gordan alipokuwa anatoa hotuba yake ambayo ilikuwa inakashifu ufisadi katika chama cha ANC, akisema kuwa huenda chama hicho hakitashinda uchaguzi wa 2019.
Umati ulianza kuimba nyimbo za kumsifu Zuma ambaye amekumbwa na kashfa baada ya nyingine.
Hafla hiyo ya Kathrada ilikuwa ikiendelea KwaZulu-Natal ambapo umati huo ulimsifu rais Zuma kwa kumpiga kalamu Gordan.