Maelfu ya raia wa Afrika Kusini wameandama katika miji mbalimbali nchini humo kushinikiza kujiuzulu kwa rais Jacob Zuma.

Shinikizo hilo linakuja baada ya rais Zuma, wiki iliyompita kumfuta kazi Waziri wake wa fedha Pravin Gordhan.

Maandamano hayo yamefanyika katika miji ya Pretoria, Johannesburg na Cape Town huku waandamanaji wakisikika wakiimba na kusema wamechoka na uongozi wa Zuma kwa sababu za ufisadi na uongozi mbaya.

Mbali na maandamano hayo yaliyotikisa nchi wabunge wa chama cha upinzani wamesema kuwa watawasilisha mswada wa kukosa imani na rais Zuma kwa madai ya ufisadi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *