Katibu mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad amesema kuwa mgogoro unaendelea ndani chao ni hujuma za CCM.
Maalim Seif amesema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu mgogoro wa CUF.
Katibu mkuu huyo amesema kuwa mgogoro unaoendelea CUF ni hujuma za Chama Tawala(CCM).
Pia ameongeza kwa kusema kuwa lengo la mkakati wa CCM sio kuimaliza CUF peke yake bali na hata kuimaliza UKAWA na upinzani kwa ujumla.
Maalim ameongeza kwa kusema kuwa hizi ni hujuma zilizopangwa na Dola ili kuua Upinzani nchini na kunyamazisha kila anayethubutu kuikosoa Serikali.
Mwisho ametoa wito kwa wazanzibari na wanaoiunga mkono CUF kusimama imara na kukilinda chama hicho kwani ieleweke kuwa Chama kinachotokea kwenye mgogoro huwa kinakuja juu sana. Nikimaliza ziara Zanzibar nitaanza jijini Dar es Salaam.