Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda amewataka mashabiki zake kutambua kuwa Shilole ni msanii mwenzake na walivyoenda Zanzibar hawakuwa pamoja kila mtu alikuwa ameenda kwa kazi yake.

Nuh Mziwanda amesema hata kama akiamua kutoka nje ya ndoa siyo lazima atoke na Shilole kwakuwa wanawake ni wengi na anapokuwa  kwenye show huwa anakutana na wanawake wengi hivyo siyo lazima atembee na Shilole.

Hata hivyo Nuh Mziwanda amesema haoni sababu ya kutoka nje ya ndoa yake na mashabiki zake wanapaswa kuelewa kwamba anapokuwa kwenye show moja na Shilole ni kutokana na maslahi hawezi kukataa pesa eti kwa sababu show aliyopata Shilole yupo.

Zanzibar kila mtu alienda kwa kazi zake japo tulijikuta tumeshukia hotel moja, Shilole akiwa ameenda kuzindua Pub lakini mimi nilikuwa nimeitwa na nimepewa pesa zangu kwa ajili ya kufanya show”.

Nuh na Shilole walikuwa wapenzi siku za nyuma kabla ya kauchana ambapo kwasasa kila mmoja ana mahusiano na mtu mwingine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *