Mwanariadha wa Kenya, Jemima Sumgong aliyeshinda medali ya dhahabu katika mashindano ya olimpiki mjini Rio mwaka jana amebainika kutumia dawa za kusisimua misuli.

Shirikisho la riadha duniani, IAAF limesema kuwa majibu waliopata kutoka katika uchunguzi wa kina katika damu ya mwaariadha huyo umeonyesha kuwa anatumia dawa za kusisimua misuli ambazo zinamsaidia kukimbia kwa nguvu na kwa muda mrefu.

Jemima Sumgong  wakati aliposhinda mbio za Rio zilizofanyika mwaka jana nchini Brazil.
Jemima Sumgong wakati aliposhinda mbio za Rio zilizofanyika mwaka jana nchini Brazil.

Mpaka sasa hakuna tamko lolote lililotolewa kutoka kwa mamlaka husika juu ya adhabu itakayotolewa baada ya majibu ya matokeo ya vipimo vya mwanariadha huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *