Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema limemkamata mtuhumiwa Musuguri David (29) anayedaiwa kumuua mpenzi wake Samira Masoud (34) kwa kumchinja kisha mwili wake kuwekwa katika jaba la maji kisa wivu wa mapenzi maeneo ya Kibamba.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro mbele ya waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi Kamishna Simon Sirro amesema katika mahojiano na mtuhumiwa huyo, amekiri kutenda kosa hilo mnamo Machi 7 mwaka huku akidai kuwa alifikia uamuzi huo baada ya kumfumania aliyekuwa mpenzi wake wakiwa chumbani na mwanaume mwingine ambaye hata hivyo mwanaume huyo alifanikiwa kutoroka.

Alieleza kuwa baada ya kifanikisha adhima yake mtuhumiwa huyo ya mauaji aliwatumia ndugu wa marehemu ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu (sms) akitumia namba ya simu ya marehemu akisema;

“Nendeni mkachukue maiti ya ndugu yenu itaozea ndani”

Kamda Sirro amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo unaendelea na utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *