Baada ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmorapa kuandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa anampenda Wema Sepetu na yupo tayari kufunga nae ndoa, Muigizaji huyo amemjia juu na kumpa makavu rapa huyo.
Wema ametumia ukurasa wake wa Instagram kumpa makavu yake rapa huyo mwenye vituko vya ajabu katika mitandao ya kijamii.
Alichokiandika Wemba Sepetu
Sijawahi kumchukia yeyote anayehangaika kutafuta riziki yake kwa kuwa nami pia natafuta. Ila mdogo wangu Harmorappa u are getting too much. Pigana na namna utakavyo kupeleka muziki na jina lako juu but get me out of this. Nakuheshimu kama msanii mwenzangu lakini hili la kunadi kunitaka kimapenzi na kuonyesha utayari wa kufanya mambo kadha wa kadhaa kwangu please waambie wengine unaodhani mnawezana ila mimi sio wa aina hiyo. Usiiharibu image yangu niliyoipigania muda wote, usiniharibie heshima yangu ninayoijenga sasa ktk chama changu CHADEMA, usiniharibie kwenye familia yangu, marafiki zangu na usiniharibie kwa niliye nae. Ni utoto na ujinga kuposti kila uchao picha za wanawake eti wanakutaka au unatoka nao *DO U THINK NAMI NI WA AINA HIYO?* Usidharaulishe. Nadhani kuna busara ya wewe to look for another one but *AM NOT FOR U* and i hope utanipa heshima yangu kama dadaako, msanii mwenzako *LETS STOP THERE*