Watu 9 wanasadikiwa kupoteza maisha huku 44 waliokolewa baada ya mashua yao ya uvuvi kuzama nje ya pwani ya kisiwa cha Zanzibar.
Makarani Mohamed, ambaye ni kaimu mkurugenzi ya kitengo cha ujajususi amesema kuwa shughuli ya kutafuta na kuwaokoa watu bado inaendelea.
Amesema kuwa “Tunafahamu, kuwa ajali hiyo ilisababishwa na upepo na mawimbi makali yaliyosababisha mashua hiyo kuzama.
Manusura mmoja waliwaambia waokoaji kuwa takriban watu 53 waliondoka kuenda kuvua samaki jana jioni wakati bahari ilikuwa tulivu.
Lakiki hali ya hewa ilibadilika na kusababisha mawimbi makali ya bahari na mpaka kupelekea kupotea kwao.
Uvuvi ni shughuli kubwa ya kiuchumi katika kisiwa cha Zanzibar lakina mashua nyingi huwa zimechakaa hali ambayo husababisha ajali nyingi.