Kikosi cha Simba kimeshawasili mkoani Mwanza kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Mbao FC utakaopigwa Aprili 10 mwaka huu.
Mratibu wa Simba, Abasi Ally alisema kwamba kwa sasa nguvu zao wanazielekeza kwenye mechi zote ambazo zimesalia ikwemo dhidi ya Mbao FC na nia yao kuona wanaibuka na ushindi kwenye mechi zote.
Abasi alisema kwamba kwa sasa bado wana ndoto za kuwa mabingwa wa ligi kuu,kwani mechi bado zimesalia na lolote linaweza kutokea licha ya kuwa nyuma kwa pointi moja na anaeongoza ligi.
Hata hivyo alisema kwamba anaamini mashabiki wa Simba bado wana imani na kikosi chao,hivyo kwa sasa ni vyema wakaelekeza nguvu zao kwenye mechi zote za ligi ambazo zimesalia.
Kabla ya mchezo huo dhidi ya Mbao FC, Simba huenda wakacheza mechi za kirafiki mkoani Geita, na baada ya hapo watakuwa na mechi ya ligi dhidi ya Toto Africans.