Taasisi ya ufuatiliaji wa mawasiliano ya internet ya ‘Internet Watch Foundation (IWF)’ yenye makao makuu nchini Uingereza imetoa ripoti na kudai Ulaya inaelekea kuwa kituo cha kumiliki picha na video zenye maudhui ya unyanyaswaji wa kingono kwa watoto.
Shirika hilo limegundua kuwa 60% ya maudhui ya unyanyaswaji wa kingono kwa watoto kwa sasa yanapatikana Ulaya, hiyo ikiwa ni ongezeko la 19%.
Ripoti hiyo imeonyesha kuwa nchi ya Uholanzi ndiyo inayoongoza miongoni mwa taifa ya Ulaya kwa kuwa na maudhui yanayokatazwa kisheria huku nchi nyingine za Ulaya zinazodaiwa kuwa na asilimia kubwa ya maudhui hayo zikiwa ni Urusi na Uturuki.
Shirika hilo la IWF limedai kuwa kuimarishwa kwa utolewaji wa taarifa na sera zinazoongoza watoa huduma za Internet kwenye bara la America Kaskazini kumechangia kutokea kwa mabadiliko hayo.
Mwaka 2015, karibu 57% ya kurasa za tovuti zilikuwa na maudhui ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto Marekani Kaskazini lakini mwaka 2016 hali hiyo ilishuka hadi kufikia 37%.