Rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameshangiliwa kwa zaidi ya dakika 10 baada ya kuingia bungeni leo mjini Dodoma.
Hatua hiyo imekuja baada ya spika wa bunge, Job Ndugai kumtangaza Kikwete kuwa ndiyo mgeni rasmi wa Bunge hilo lililoanza leo mkoani Dodoma.
Dkt. Jakaya Kiwete aliudhuria kuapishwa kwa mke wake Mama Salma Kikwete kuwa mbunge wa kuteuliwa ambapo leo amekula kiapo cha utii.
Wabunge hao wameonesha furaha yao kwa rais huyo mstaafu huku wabunge wengine wakisema kuwa wamemmsi Kikwete huku wengine wakisikika wakisema kuwa rudi tena mkuu.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema kuwa toka aingie bungeni kipindi cha nne sasa hajawahi kuona mgeni anapigiwa makofi na kushangiliwa kama alivyofanyiwa Kikwete leo.
Ndugai aliwataka wabunge hao wasimame na kumpungia mikono Kikwete wakati akiwa sehemu maalum za kukaa wageni bungeni hapo.