Mke wa rais mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Salma Rashid Kikwete ameapishwa kuwa mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mh.Salma aliandamana na mumewe rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete, ambaye uwepo wake ulisababisha kelele za shamra shamra kutoka kwa wabunge wakisema kwa sauti ‘tumekumiss tumekumiss’.

Mama Salma Kikwete eliteuliwa kuwa mbunge wa viti maalumu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.

Mkutano wa saba wa bunge la Tanzania umeanza kikao chake cha kwanza cha mkutano wa bajeti hii leo.

Mama Salma kama anavyotambulika na wengi nchini ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM, lakini pia anatajwa kuwa na ushawihi mkubwa sana wa kisiasa ndani ya chama chake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *