Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dk Anna Makakala amefanya mabadiliko makubwa ya viongozi wa Uhamiaji wa mikoa mbalimbali nchini na kuwateua wakuu wapya wa mikoa Bara na Visiwani.

Alitoa mfano kuwa mwaka jana, Tanzania ilipata ugeni wa waumini wa madhehebu ya Mabohora waliofanyia sherehe yao kubwa nchini. Alisema sherehe hizo kwa kuwa zilikuwa za kimataifa wageni wapatao 32,000 waliingia nchini kuja kusherehekea sikukuu hiyo.

Amesema ukipiga hesabu ya kila mmoja ni wazi kuwa walilipa fedha za kutosha; lakini cha ajabu ni kwamba alipouliza fedha kiasi gani zilipatikana kutokana na ugeni huo mkubwa, hadi hadi hajapatiwa hesabu yoyote jambo linalodhihirisha kwamba kuna matatizo makubwa katika Idara ya Uhamiaji.

Kabla ya mabadiliko makubwa, Dk Makakala aliteua makamishna sita ambao ni Peter Chogero ambaye ni Kamishna wa Divisheni ya Fedha na Utawala, Samwel Magweiga (Kamishna wa Divisheni ya Udhibiti na Uongozi na Mipaka), Gerald Kihiga (Kamishna wa Divisheni ya Pasipoti na Uraia), Musanga Etimba (Kamishna wa Divisheni ya Hati za Ukaazi na Pasi) na Hannerole Manyanga ambaye ni Kamishna wa Divisheni ya Sheria.

Lakini jana, Dk Makakala alitangaza mabadiliko mengine makubwa ambayo yameshuhudia Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Sixtus Nyaki aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mwanza akihamishiwa Mkoa wa Simiyu wakati aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Rukwa, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Selemani Kameya amehamishiwa Tabora.

Taarifa iliyotolewa na Kamishna Jenerali huyo inaonesha kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mbeya, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Asumsio Achacha amehamishiwa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Manyara, Naibu Kamishna Peter Kundy amehamishiwa Mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi, Ali Mohamed ambaye amehamishiwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Arusha.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *