Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Harmorapa usiku wa jana amekoswa kupigwa na chupa wakati akitumbuiza kwenye show ya Diana Nyange ‘Usiku wa Komela’ katika ukumbi wa Maisha Basment jijini Dar es Salaam.
Harmorapa ambaye katika show hiyo alitokea kama mgeni mwalikwa, alipata nafasi ya kuwasalimu mashabiki wake na kufanya show kidogo lakini wakati rapa huyo akifanya yake stejini alijitokeza kijana mmoja na kurusha chupa huku akiwa na lengo la kutaka kumpiga msanii huyo.
Harmorapa ni kama aliwahi kuiona ile chupa na kubahatika kuikwepa hivyo haikuweza kuleta madhara ya moja kwa moja kwa msanii huyo ila sauala hili lilipelekea msanii huyo kushindwa kuendelea kufanya show.
Akiwa stejini anaperform wimbo wake mpya ‘Kiboko ya mabisho’, Harmo Rappa alijikuta akirushiwa chupa iliyokuwa na bia na moja ya mashabiki waliohudhuria show hiyo kisa mstari mfupi unaosikika kwenye wimbo wake; “Tulikuwa WASAFI kabla ya WCB, maneno yao machafu hayaniharibii CV.
Kwa upande wa meneja wa Harmorapa, Irene Sabuka alifunguka na kusema kama Harmorapa asingeweza kukwepa ile chupa au kwa bahati mbaya ingemkuta saizi huenda tungekuwa tunazungumza mambo mengine kwenye jambo hilo.