Makamu wa Rais a chama cha wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Godwin Ngwilimi amekamatwa na polisi huko mkoani Shinyanga na anashikiliwa katika kituo kikuu cha polisi mkoani humo.
Taarifa iliyotolewa na Rais wa TLS Mhe.Tundu Lissu ni kwamba Ngwilimi akiwa katika gari yake alisimamishwa na askari aliyekua kavaa kiraia, akitaka kukagua gari yake.
Ngwilimi alimtaka Askari huyo ajitambulishe kwanza kwa kutoa kitambulisho cha kazi kabla ya upekuzi.
Lakini badala ya kujitambulisha alimzuia Ngwilimi na kumuelekeza kituo kikuu cha polisi Shinyanga ambapo anashikiliwa hadi sasa.
Katika kuvutanavutana ikabidi wapelekane kituo cha Polisi Shinyanga. Alipofika Wakataka Kusearch bado akakataa akawataka aje OCD, OCCID, RPC au RPO ndipo wamkague.
Mwisho wake akapatikana mmoja ya hao aliowataka baada ya kusubiri muda mrefu, alivyokuja akaandika Search warrant na kuanza kumkagua.
Hawajapata chochote, hata gari lake halikuwa na Kosa lolote. Kwakuwa habari zilikuwa zimeshaaenea kwenye Mitandao ya Kijamii, Pia huyu Wakili ni Mwalimu wa sheria na amewafundisha baadhi ya Polisi waliokuwa Pale, Baadhi yao wakamtambua, wakaja kugundua kumbe waliyemkamata ni Makamu wa Rais wa chama cha wanasheria Tanganyika (TLS).
Wakamuomba msamaha na kumwambia hawakujua. Wakamuomba radhi kwa kumchelewesha Safari yake. Ndipo wakamuachilia bila mashariti yoyote akaondoka zake mida ya saa nne usiku kuelekea Saa tano za usiku.