Wanasayansi wamethibitisha kuwa mitandao ya kijamii ndicho chanzo cha magonjwa mbali mbali yakiwamo ya akili na kulemaa kwa mishipa ya shingo.

Wasayansi hao wamesema kuwa mitandao ya kijamii kama vile Facebook, Twitter WhatsApp, Instagram na michezo ya kwenye Internet usababisha magonjwa ya akili, uraibu na maumivu ya shingo na mgongo kutokana na kuinama kila wakati wakati wa kuchati.

Tovuti ya Neck Institute (London) imeeleza kuwa madhara ya shingo na Uti wa mgongo yanayosababishwa na matumizi ya simu kwa muda mrefu hasa kwa kuandika ujumbe mfupi ambapo uhathiri mamilioni ya watu duniani.

Daktari bingwa wa neva za fahamu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja amesema kuwa bado hakuna ushahidi wa kisayansi kama  matumizi ya simu yanaathiri mishipa ya shingo lakini yanaathiri misuli.

Profese Mtuja amesema kuwa kuinamia simu muda mrefu kunasababisha maumivu ya shingo, mgongo pamoja na kichwa.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *