Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amedai kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Profesa Lipumba anatumiwa kukihujumu chama ili kishindwe kudai haki iliyopata kwenye uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka juzi.

Maalim Seif ameyasema hayo jana katika kijiji cha Tumbatu, Mkoa wa Kaskazini Unguja alipokuwa anazungumza na wanachama wa chama hicho katika ziara yake ya kuhimarisha chama hicho mjini Unguja.

Katibu mkuu huyo amesema kuwa licha ya Profesa Lipumba kupata nguvu kutoka vyombo dola pamoja na ofisi ya msajiri wa vyama vya siasa nchini ili kukihujumu chama hicho lakini hatoweza kufikia malengo yake.

Pia amesema kuwa Taasisi hizo kwa pamoja zimekuwa zikimuunga mkono Lipumba kwa kumpa kila nguvu anayohitaji ili kuona anafanikisha malengo ya CCM ya kuitawala nchi bila kuwepo na chama pinzani chenye nguvu.

Maalim Seif amesema kuwa anashangaa kuona vyombo vya dola pamoja na ofisi ya msajiri wa vyama bila kufuata Katiba na Sheria za nchi wao wamekuwa wakikihujumu chama hicho.

Kuhusu kuvuliwa nafasi ya ukatibu, Maalim Seif amesema kuwa Lipumba hana uwezo wa kumvua cheo hicho hata kama angekuwa Mwenyekiti halali kwasababu katibu mkuu anaondolewa mpaka mkutano mkuu uhudhuriwe na nusu ya wajumbe.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *