Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Ally Hassan Mwinyi amemuomba kiongozi wa dini ya Wahindu ya Swaminarayan Duniani, Mahant Swami Maharaji kuiombea Tanzania amani na umoja viweze kudumu na kusiwepo aina yoyote ya ubaguzi kwa sasa na hata vizazi vijavyo.

Mwinyi aliyasema hayo Dar es Salaam baada ya kualikwa katika hafla ya kumkaribisha kiongozi huyo hapa nchini na kukutana na waumini wa dini hiyo.

Pia ilikua ni maadhimisho ya miaka 40 tangu kujengwa misikiti miwili ya dini hiyo hapa nchini.

Alishukuru kwa kualikwa katika hafla hiyo ya kidini kwani sio jambo la kawaida kupokea ugeni wa kiongozi wa kidini nchini.

Alimkaribisha kiongozi huyo nchini na kumtaka kuiombea sana Tanzania ili iendelee kudumisha amani na umoja na licha ya kutokuwepo kwa aina yoyote ya ubaguzi, aendelee kuomba ili hali hiyo isiwepo kamwe na wananchi waendelee kuishi kama ndugu.

Kwa upande wake, kiongozi huyo ambaye ni wa sita kwa nafasi hiyo, Maharaji alisema ataendelea kuiombea Tanzania na dunia nzima kwa ujumla ili wananchi wake waendelee kubarikiwa katika maisha yao pamoja na kukuza maendeleo yao.

Alisema mwanadamu siku zote hupenda raha lakini ni vyema wakafahamu kuwa hakuna raha kubwa kama kupata kutoka kwa Mungu kwa kuwa raha nyingine zote ni za muda, hazidumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *