Mfanyabiashara Erick Shigongo amemshauri Alikiba kuhusiana na muziki wake ili hata siku asipokuwepo kwenye ramani ya muziki awe na maisha yenye tija kulingana na kazi alizofanya nyuma.

Erick Shigongo ameamua kuwakumbusha vijana pamoja na watanzania kiujumla kuwa siku zote unapopata mafanikio fulani katika nyanja yoyote ile yale mafanikio huwa yamechangiwa na baadhi ya watu ambao unapaswa kuendelea kuishi nao vyema pasipo kuwatenga maana wao ndiyo wameweza kukupa mafanikio hayo.

 “Kwanza kabisa nianze kwa kukiri kuwa sikuwahi kukutana na Alikiba ana kwa ana mpaka miezi miwili iliyopita nikiwa katika Hotel ya Double Tree, iliyopo Masaki, Jijini Dar es salaam. Nilikwenda pale kwa ajili ya chakula cha mchana na mke wangu. Muda mfupi tu baada ya sisi kuingia walifika Alikiba na meneja wake Christine Mosha (Seven) wakaja moja kwa moja kwenye kona tuliyokaa na kutusalimia. Kitu cha kwanza nilichojifunza na kukipenda kwa Alikiba ni unyenyekevu, kijana huyu ni mnyenyekevu mnoooo! Kitu hiki peke yake ukiachana na muziki wake kilinifanya nimpende Kiba. Walipoondoka mimi na mke wangu wote tulikiri KIBA NI MNYEYEKEVU NA NDIYO SABABU AMEFANIKIWA SANA KATIKA MUZIKI”.

Mbali na hilo Shigongo anasema katika maisha hakuna mtu anaweza kuwa mshindi siku zote, wala hawezi kuwa bora kila wakati kwani kila jambo huwa lina wakati wake, hivyo anamuasa Alikiba atambue kuwa hawezi kuwa na nafasi hiyo kila siku, hivyo anapaswa kujipanga na kutowadharau wale waliompandisha na kufikia hapo alipo.

 “Alikiba, meneja wake na Watanzania wenzangu lazima mnisikilize hapa; MAFANIKIO MAISHANI HUJA NA KITU NYUMA YAKE, mara nyingi kitu hicho huwa kuwapuuza na kuwadharau waliokufikisha ulipo. Kuwatenga bila kufahamu hao ndiyo wanunuzi wa kazi zako ama wasikilizaji wa muziki wako na wakikuachia tu utatumbukia shimoni na huo ndiyo utakuwa mwisho wako. Ali kiba anapaswa kufahamu kwamba hawezi kuwa Champion for life, hata akiwa bora kiasi gani lazima siku moja atakuja mtu bora zaidi yake. Kabla ya Chris Brown alikuwepo Usher Raymond, kabla ya Rihanna alikuwepo Beyoncé, kabla ya Floyd Maywether alikuwepo Mike Tyson, kila zama na bingwa wake. Leo ni Kiba kesho atakuwa mwingine”.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *