Madaktari nchini Kenya, wamefanikiwa kuishawishi mahakama nchini humo kuzuia kuajiriwa kwa madaktari 500 kutoka Tanzania.

Madaktari hao walienda mahakamani kuizuia serikali ya nchi hiyo kutoa ajira hizo wakidai kuwa kuna madaktari 1,400 wasio na ajira nchini humo.

Wamelalamika kuwa itakuwa ni ufujaji wa fedha kuwa na madakrari 500 wa Kitanzania watakaolipwa tshs 360,000 kwa siku. Mahakama ya kazi imetoa agizo hilo Ijumaa jii (March 31), ikisema kuwa litadumu hadi ombi la maofisa wa afya litakaposikilizwa na kuchambuliwa.

Mahakama hiyo imetoa siku 21 kwa serikali kuwajibu maofisa hao na suala hilo litatajwa April 19.

Mwezi huu Rais Dkt John Magufuli alisema kuwa Tanzania itapeleka madaktari 500 kukabiliana na uhaba uliopo na tangazo la nafasi hizo lilitolewa kuwataka wenye sifa kutuma maombi.

Hata hivyo mpango huo umepingwa vikali na baadhi ya viongozi wa nchini humo akiwemo Raila Odinga, ambaye ni rafiki wa karibu na Rais Magufuli.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *