Hoteli ya kifahari nchini Kenya, inayomilikiwa na raia wa Italia na mwandishi wa vitabu Kuki Gallmann, imechomwa moto na watu wanaokisiwa kuwa wafugaji.
Hilo ndilo shambulizi la hivi punde katika eneo hilo linalokumbwa na ukame la Laikipia, kutoka kwa watu wanaikisiwa kuwa wafugaji ambao wanavamia mashamba ya kibinafsi wakitafuta malisho.
Hakukuwa na wageni ndani ya hoteli hiyo ya Mukutan wakati ilipochomwa moto na wafugaji hao nchini Kenya.
Mapema wiki hii, polisi wanaripotiwa kuwapiga risasi na kuwaua karibu ng’ombe 100 katika shamba linalomilikiwa na Bi Gallmann.
Eneo la Laikipia lenye ukubwa wa ekari 10,000, mraba ndiko wazungu humiliki mashamba makubwa.