Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ amesema kuwa hajagombana na mpenzi wake Spicy kutoka Nigeria na wapo vizuri kama zamani.

Jide amefunguka hayo baada ya kuenea taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa wawili hao wamegomba na hawapo kwenye mahusiano.

Mwanamuziki huyo amesema kuwa wabongo wengi wanapenda wenzao waharibikiwe na kuwataka kuacha kuwaziana mabaya badala yake waombeane mema.

Jide amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya maneno kuzagaa kuwa amepigana kibuti na Mnigeria huyo ikiwa ni siku wiki chache baada ya kuandika maneno yaliyomo kwenye wimbo wa  Rosella katika mtandao wa Instagram.

 Kwa upande mwingine Lady Jaydee atarajia kuzindua albamu yake ya saba tarehe kesho katika ukumbi wa Lugalo uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *