Waandaaji wa tuzo kubwa za filamu duniani za Oscars wameridhia kuendelea kufanya kazi na kampuni ya uhasibu ya PricewaterhouseCoopers (PwC) licha ya kampuni hiyo kuvurunda kwenye tuzo za mwaka huu.
Kampuni ya PwC imekubali lawama zote kwa kosa ‘lisilokubalika’ ambalo lilipelekea filamu ya La La Land kutangazwa kimakosa kama mshindi wa tuzo badala ya filamu ya Moonlight.
Rais wa Oscars, Cheryl Boone Isaacs, ameandika barua kwa wahusika wote kuwa kanuni mpya pia zitazuia wafanyakazi kutumia vifaa vya kielektroniki wanapokuwa nyuma ya pazia wakiendela na shughuli za kikazi.
Afisa wa PwC, Brian Cullinan alikutwa akituma picha kwenye mtandao wa Twitter muda mfupi kabla ya kuchanganya matokeo kw akumpa staa wa filamu Warren Beaty bahasha tofauti na hivyo kuchanganya matokeo.