Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam imemuachia huru Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali baada ya kukubaliana na warufani kwamba hati ya mashtaka iliyomtia hatiani ilikuwa na upungufu.

Uamuzi huo umetolewa leo mbele ya Jaji Ama- Isaria Munisi baada ya kupitia sababu za kupinga mbunge huyo kutiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela.

Lijuakali aliwakilishwa mahakamani na Wakili Tundu Lissu na Fred Kiwelo wakati Jamhuri ilikuwa ikiwakikishwa na Wakili wa Serikali, Faraja Nchimbi.

Mshtakiwa mwingine aliyehukumiwa kifungo cha nje, Stephani Mgatta adhabu yake pia imetenguliwa.

Mahakama ya wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro ilimhukumu mbunge huyo kwenda jela miezi sita bila faini baada ya kukutwa na hatia ya kuwafanyia fujo polisi wakati wa Uchaguzi Mkuu  mwaka 2015.

Mbunge huyo na dereva wake, John Bikasa walikutwa na hatia ya kukata utepe wa polisi na kuwafanyia fujo jambo ambalo ni kinyume na sheria.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *