Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu leo anatarajia kuzindua ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza dawa za binadamu kilichopo Zinga wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani.
Kiwanda cha Zinga Pharmaceuticals LTD uzinduzi wa ujenzi huo unatarajiwa kufanywa leo kwa kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa wilaya ya Bagamoyo.
Miongoni mwa viongozi watakaohudhuria uzinduzi wa ujenzi huo ni mbunge wa Bagamoyo mkoani Pwani, Dkt. Shukuru Kawambwa.
Kiwanda hicho kitatengeneza dawa zenye standard ya Europe na kitakuwa na uwezo wa kusambaza dawa hizo Afrika Mashariki na Kati kitakapokamilika.
Mitambo itakayozalisha dawa hizo itatoka Ujerumani na tayari wataalam wake wameshaingia nchini kwa ajili ya kuanza kufanya kazi hiyo muhimu.
Ujenzi wa kiwanda hicho cha dawa za binadamu utafaidisha nchi kuelekea uchumi wa viwanda ikiwa ni ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuinua sekta ya viwanda nchini.